Mpanda FM

Zaidi ya vijana  500 Katavi wanufaika na mradi wa Agri­–Connect

27 November 2024, 4:07 pm

picha ya mtandaoni

 

Lengo la mradi ilikuwa ni kuhamasisha vijana kuingia katika shughuli za uzalishaji wa mbogamboga na matunda.

Na Rachel Ezekia-Katavi

Zaidi ya vijana  500 mkoani Katavi wamenufaika na mradi wa Agri ­–Connect katika  kilimo cha uzalishaji wa mazao yatakayosaidia kupunguza udumavu    na kuongeza lishe bora kwa kina mama wajawazito.

Hayo yamebainishwa na  Frank Kamnyoge mratibu wa  mradi wa Agri –Connect  mkoa  wa Katavi  wakati akiwasilisha  mipango kazi ya mradi  ambapo lengo la mradi ilikuwa ni kuhamasisha vijana kuingia katika shughuli za uzalishaji wa mbogamboga na matunda.

Sauti ya mratibu wa  mradi wa Agri –Connect  mkoa  wa Katavi Frank Kamnyoge

Kwa upande wake Nehemia james katibu tawala  Msaidizi mkoa wa Katavi  uchumi na uzalishaji  katika kikao hicho   amewataka maafisa ugani na maafisa lishe kwenye  ngazi ya halmashauri kuendeleza na kusimamia  na kutekeleza mradi huo na kuwataka vijana kuwa wabunifu  ili kuwasaidia katika uzalishaji.

Sauti ya katibu tawala  Msaidizi mkoa wa Katavi 

Moja ya vijana mnufaika wa mradi wa agri-connect manispaa ya Mpanda amebainisha fursa aliyoipata kupitia mradi huo kuanzia kwenye uzalishaji hadi upelekaji wa mazao katika soko huku akishauri vijana kutumia fursa ya kilimo katika kujikwamua kiuchumi.

 Moja ya vijana mnufaika wa mradi wa agri-connect manispaa ya Mpanda

Mradi wa Agri –Connect   ulioanza mwaka 2020 na umefika tamati mwaka huu 2024 .