Madereva bajaji Katavi kutotumika kuvunja amani wakati wa uchaguzi
25 November 2024, 1:40 pm
“wajibu wao kuhakikisha hawatumiki kipindi hichi cha uchaguzi wa serikali za mitaa kuvunja amani .“
Na Lilian Vicent – Katavi
Madereva bajaji Kituo cha soko kuu Manispaa ya Mpanda Mkaoni Katavi wamesema katika kipindi cha kampeni hawatakubali kutumika kuvunja amani.
Hayo yamejiri katika kikao cha mrejesho wa maagizo Katika kikao na mkuu wa mkoa wa Katavi pamoja na viongozi wa makundi mbalimbali ikiwemo bajaji katika ukumbi wa manispaa November 13 mwaka huu.
sauti za madereva bajaji
Frank Kalotho ambaye mwenyekiti wa umoja huo wa bajaji amesema ni wajibu wao kuhakikisha hawatumiki kipindi hichi cha uchaguzi wa serikali za mitaa kuvunja amani .
Sauti ya mwenyekiti wa umoja wa bajaji mkoa wa Katavi
Nae mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko katika kikao hicho amesema kuwa waendesha vyombo vya usafiri kama bajaji wanakutana na watu wengi hivyo wakigundua viashiria vya uvunjifu wa amani watoe taarifa.
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko
Kampeni za uchaguzi wa serikali wa mitaa zimeanza November 20 hadi November 26 ambapo kauli mbiu ya uchaguzi wa serikali za mitaainasema ‘ Serikali za mitaa ,sauti ya wananchi jitokezee kushiriki uchaguzi’.