Katavi: watu 6 wapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kipindupindu
20 November 2024, 5:36 pm
“Jumla ya wagonjwa 6 wameripotiwa kupoteza maisha wagonjwa 419 tayari wamesharuhusiwa huku wengine 16 wakiwa bado kwenye uwangalizi “
Na John Benjamin -Katavi
Watu 441 wameripotiwa kuwa na ugonjwa wa Kipindupindu katika tarafa ya Karema kata ya Ikola halmashauri ya wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.
Akiwasilisha taarifa katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa katavi katibu tawala mkoa wa Katavi Albert Msovela amesema Septemba 13 hadi Novemba 18 jumla ya wagonjwa 6 wameripotiwa kupoteza maisha wagonjwa 419 tayari wamesharuhusiwa huku wengine 16 wakiwa bado kwenye uwangalizi
Sauti ya katavi katibu tawala mkoa wa Katavi Albert Msovela
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa wa Katavi waliohudhuria katika kikao hicho wameiomba wakala ya maji vijijini Ruwasa kuhakikisha inafikisha huduma ya maji safi katika shule zote za msingi na sekondari ili kupunguza mlipuko wa ugonjwa huo wa kipindupindu.
Sauti ya wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa wa Katavi waliohudhuria katika kikao
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewaagiza wataalamu wa afya ,wakuu wa idara kuweka mikakati na usimamizi wa namna ambavyo ugonjwa wa kipindupindu utatokomezwa katika mkoa.
Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko
Katika kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu kambi kwa ajili uratibu wa shughuli za matibabu naufuatiliaji ilifunguliwa mara baada ya kuthibitisha uwepo wa mlipuko kambi hiyo iliyopo tarafa ya karema kata ya ikola imekuwa eneo muhimu la kuhimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu.