Mpanda FM

Katavi: Wakazi kata ya Majengo walalamikia kutozolewa taka kwa wakati

6 November 2024, 7:13 pm

Takataka zilizopo katika moja ya nyumba kata ya majengo.picha na Samwel Mbugi

Kampuni ambayo inajihusisha na uzoaji wa taka hizo, kutokana na uchache wa vifaa jambo hilo  limesebabisha mrundikano wa takataka katika makazi yao

Na Samwel Mbugi -Katavi

Wananchi wa kata ya majengo manispaa ya Mpanda walalamikia kuhusu mrundikano wa takataka katika makazi na kuhofia magonjwa ya mlipuko yatokanayo na uchafu wa mazingira.

Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na mpanda radio fm kuwa taka hizo zimekuwa kero kwao kwani zimesababisha harufu mbaya katika makazi yao wanayoisha.

Sauti za Wananchi wa kata ya majengo

Kwa upande wake mtendaji wa kata hiyo Tarcius Mchina amesema kuwa kuna kampuni ambayo inajihusisha na uzoaji wa taka hizo, kutokana na uchache wa vifaa jambo hilo  limesebabisha mrundikano wa takataka katika makazi yao

Sauti ya mtendaji wa kata hiyo Tarcius Mchina

Hata hivyo Mchina ametoa wito kwa wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kwana changamoto hiyo inakwenda kutatuliwa pindi watakapokuwa wamepata vitendetea kazi vitakavyosaidia katika ukusanyaji wa takataka.