Mpanda FM

Madiwani Katavi wakerwa kutotatuliwa changamoto wanazowasilisha

6 November 2024, 6:50 pm

picha na John Benjamin

“Wameeleza kuwa kumekuwepo na kujirudia kwa changamoto kila kikao kama ukosefu wa choo cha  machinjio kata ya Mpanda Hoteli mgogoro wa mwekezaji kata ya Magamba na sehemu ya maegisho ya magari makubwa mjini hali ambayo imekuwa kero. “

Na John Benjamin-Katavi

Baadhi ya madiwani katika halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia kutokufanyiwa kazi kwa changamoto ambazo wamekuwa wakiwasilisha katika vikao vya baraza la madiwani.

Hayo yamejili katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya mwaka 2024/2025 ambapo wameeleza kuwa kumekuwepo na kujirudia kwa changamoto kila kikao kama ukosefu wa choo cha  machinjio kata ya Mpanda Hoteli mgogoro wa mwekezaji kata ya Magamba na sehemu ya maegisho ya magari makubwa mjini hali ambayo imekuwa kero. 

Sauti za baadhi ya madiwani

Kaimu mkurungezi wa halmashauri ya manispaa Mpanda Deodatus Kangu amesema kuwa halmashauri ya manispa ya Mpanda imekuwa ikifanyia kazi maazimio na maagizo yote ambayo yamekuwa yakitolewa katika vikao vya baraza hilo huku akitoa ahadi ndani ya siku 30 choo kitakuwa kimeshajengwa katika eneo la machinjio hiyo.

Sauti ya Kaimu mkurungezi wa halmashauri ya manispaa Mpanda Deodatus Kangu

Kwa upande wake Mstahiki meya wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Hidary Sumry amewataka wakuu wa idara ambao wamekuwa wakihudhuria baraza hilo kuhakikisha wanafanyia kazi changamoto ambazo zinajitokeza kwenye idara zao ili kuhakikisha changamoto zote ambazo zinawasilishwa na madiwani zinatatuliwa.

Mstahiki meya wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Hidary Sumry

Mstahiki meya wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Hidary Sumry.picha na John Benjamin

Kikao cha robo ya mwaka wa 2024/2025 cha baraza la madiwani kimelenga kusikiliza taarifa na changamoto ya kata zote 15 zilizopo katika halmashauri ya manispaa ya Mpanda.