Katavi:TAKUKURU yafuatilia miradi 33 yenye thamani ya Bilion 46
4 November 2024, 2:13 pm
kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Stuart Kiondo .Picha na Samwel Mbugi
“sekta zilizofuatiliwa ni elimu, kilimo, afya, Uchumi biashara na miundombinu“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Katavi imefanikiwa kufuatilia utekelezaji wa miradi thelathini na tatu (33) yenye thamani ya shilingi bilioni 46 kwa robo ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Hayo yamesemwa na kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Stuart Kiondo ambapo amesema sekta zilizofuatiliwa ni elimu, kilimo, afya, Uchumi biashara na miundombinu.
Sauti ya kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Stuart Kiondo
kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Stuart Kiondo .Picha na Samwel Mbugi
Katika hatua nyingine taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU imefanya uchambuzi wa mifumo kwa lengo la kubaini mianya ya rushwa ambayo inaweza kupelekea vitendo vya rushwa kutokea.
Sauti ya kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Stuart Kiondo
Kiondo amewaasa wasimamizi wa miradi ya umma kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, miongozo mbalimbali ( force account ) na mingine akisisitiza umakini, ushirikiano na uzalendo ili kupata thamani ya fedha.