DC Tanganyika azindua bweni la wasichana sekondari ya Sitalike
30 October 2024, 4:33 pm
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu, picha na Lea Kamala
“Kukamilika kwa bweni kutatatua changamoto iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa kike na kuchangia kutomaliza masomo yao.”
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu kwa niaba ya Mkuu Wa Mkoa wa Katavi amezindua bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Sitalike. Kukamilika kwa bweni hilo kutatatua changamoto iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa kike na kuchangia kutomaliza masomo yao.
Akizungumza wakati akifungua bweni hilo lililojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 190 Buswelu amesema bweni hilo litapunguza utoro na visababishi vya mimba vinavyotokana na vishawishi .
Sauti ya mkuu wa wilaya Onesmo Buswelu
Naye, Naibu Kamishna wa Uhifadhi – TANAPA na Mkuu wa Kanda ya Kusini Steria Ndaga kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi – TANAPA amewataka wanafunzi hao kulitunza bweni hilo ili litumike kwa muda mrefu.
Sauti ya Kamishna wa Uhifadhi – TANAPA Steria Ndaga
Akisoma ripoti ya mradi huo wa bweni Mkuu wa Shule ya Sekondari Sitalike Samson Kaitira Mafwolo amesema, Mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 190 ambapo TANAPA ilichangia zaidi ya milioni 77, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ilichangia zaidi ya milioni 97 na DED Wilaya ya Nsimbo akichangia milioni 15.