Mpanda FM

Tuelimike yatoa elimu kwa wananchi kuelekea uchaguzi serikali za mitaa

25 October 2024, 3:11 pm

Mkurugenzi wa asasi ya Tuelimike kijiji cha isanjandugu halmashauli ya nsimbo Douglas Mwaisaka picha na Lea Kamala

” Wananchi wanapaswa  kuchagua kiongozi ambaye atakuwa tayari kushirikiana na jamii yake, mwenye nia na uwezo wa kuwaongoza.”

Na Lea Kamala

Wananchi wa manispaa ya mpanda mkoani Katavi, wameshauriwa kuchagua kiongozi bora ambaye atakuwa tayari kutatua changamoto za wananchi na kuleta maendeleo katika jamii.

Akizungumza na Mpanda Radio Fm kwa njia ya simu, mkurugenzi wa asasi ya tuelimike kijiji cha Isanjandugu kata ya Nsimbo  halmashauri ya Nsimbo Douglas Mwaisaka amesema kuwa wananchi wanapaswa  kuchagua kiongozi ambaye atakuwa tayari kushirikiana na jamii yake, mwenye nia na uwezo wa kuwaongoza.

Sauti ya Mkurugenzi wa Asasi ya Tuelimike Douglas Mwaisaka

Nao baadhi ya wananchi wa manispaa ya mpanda mkoani Katavi wamesema kuwa kiongozi bora lazima awe mtanzania, awe tayari kuwatumikia wananchi na kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali za kijamii

Sauti za Wananchi

Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi wa serikali za  mitaa novemba 27 kuchagua mwenyekiti wa serikali za mitaa, kijiji , kitongoji  na wajumbe.