Mpanda FM

Tanganyika wahimizwa kulinda miundombinu inayojengwa

25 October 2024, 2:35 pm

Daraja la Ifume, picha na mtandao

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu, amemtaka mkandarasi kuhakikisha daraja la Ifume linajengwa kwa ubora  ili liweze kuwaondolea wananchi wa maeneo hayo kero ya kutumia barabara hususani msimu wa mvua.

Wananchi wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wametakiwa kulinda miundombinu ya barabara inayoendelea kujengwa na serikali katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Moja ya mradi alioutembelea Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu ni  ujenzi wa daraja la Ifume linalounganisha vijiji vya Kapalamsenga na Itunya, daraja lenye thamani ya shilingi milioni 700  ambapo amemtaka  mkandarasi kuhakikisha daraja hilo linajengwa kwa ubora  ili liweze kuwaondolea wananchi wa maeneo hayo kero ya kutumia barabara hususan msimu wa mvua

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TARURA Tanganyika mhandisi Maila Richard Yessaya  akizungumza wakati akisoma taarifa ya mradi amesema mradi ulianza 10/05/2024 na unatarajiwa kukamilika 6/11/2024

Sauti ya Mhandisi Maila Richard Yessaya

Kwa upande wao wananchi wa maeneo hayo ambayo ndio walengwa wa miradi hiyo wakizungumza na kituo hiki wamepongeza jitihada za serikali kuendelea kuwaboreshea miundombinu mbalimbali.

Sauti za Wananchi