Mpanda FM

Wananchi mtaa wa Mpadeco Katavi walalamikia kutozolewa takataka kwa wakati

15 October 2024, 6:23 pm

Miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na Samwel Mbugi

“Taka hizo zimekuwa kero kutokana na kukaa bila kuzolewa licha ya kutoa fedha  za kutoa takataka hizo katika makazi yao.

Na Samwel Mbugi -Katavi

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda wamezitaka mamlaka kutatua changamoto  ya mrundikano wa uchafu katika makazi.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio FM  ambapo wamesema  taka hizo zimekuwa kero kutokana na kukaa bila kuzolewa licha ya kutoa pesa   za kutoa takataka hizo katika makazi yao.

Sauti za wananchi mtaa wa Mpadeco wakizungumzia kero ya uchafu katika mtaa wao

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mpadeco Ivo Chambala amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambayo inasababishwa na uchache wa magari ya kubeba taka pamoja na ubovu wa miundombinu ya Barabara kuwa ni moja ya sababu zinazosababisha mrundikano mkubwa wa takataka.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Mpadeco Ivo Chambala

Hata hivyo jitihada zinaendelea kufanyika ili kuwapata wenye mamlaka husika ambao wanaweza kutolea ufafanuzi  dhidi ya changamoto hizo

Sambamba na hilo   mwenyekiti Chambala amewataka Wananchi wa mtaa wa Mpadeco kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la wakazi litakalotumika November 27 mwaka huu kuchagua viongozi wa serikali za mitaa.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Mpadeco Ivo Chambala