Mpanda FM
Wazee Katavi waomba kuimarishiwa huduma za afya
10 October 2024, 4:58 pm
baadhi ya wazee manispaa ya Mpanda
“Kuwepo na msisitizo juu ya matibabu ya bure kwa wazee wasiojiweza kumudu gharama za matibabu.“
Na Lazaro Maduhu-Katavi
Baadhi ya wazee wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuhimarishiwa huduma ya matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio FM kwa nyakati tofauti wakidai kuwepo na msisitizo juu ya matibabu ya bure kwa wazee wasiojiweza kumudu gharama za matibabu.
Nae Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Mpanda Thabiti Malagano amesema serikali imeshatoa msamaha kwa wazee juu ya matibabu huku akitoa utaratibu wake kwa wanufaika hao jinsi ya kupatiwa huduma hiyo bure.