Mpanda FM

Wananchi Katavi watakiwa kuzingatia unywaji maji ulio sahihi

24 September 2024, 9:16 pm

picha na mtandao

Kitaalamu unywaji wa maji unatofautiana kulingana na jinsia; wanawake, wanaume na watoto kuzingatia unywaji huo husaidia zaidi mzunguko mzuri wa damu,

Na Rachel Ezekia -Katavi

Wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia viwango sahihi vya unywaji wa maji kama ambavyo inashauriwa na wataalam wa afya ili kujilinda na kuepukana na changamoto zinazotokana na ukosefu wa maji mwilini.

Wito huo umetolewa na Dkt. Paul Lugata mganga mfawidhi  hospitali  ya wilaya ya Mpanda ambapo amesema kuwa kitaalam unywaji wa maji unatofautiana kulingana na jinsia wanawake, wanaume na watoto na kwamba kuzingatia unywaji huo husaidia zaidi mzunguko mzuri wa damu,kulainisha maungio ya viungo mwilini.

Sauti ya Dk. Paul Lugata mganga mfawidhi  hospital  ya Wilaya ya Mpanda

Ameongeza kuwa maji husaidia kutoa uchafu na kuzuia baadhi ya magonjwa pamoja na ubongo kufanya kazi vizuri ,amebainisha madhara ya kutotumia maji husababusha magonjwa ya moyo ,Figo, maumivu kwenye viungo vya mwili ambapo amewataka wananchi kuwa na mazoea ya kunywa maji ndani ya masaa 24.

Sauti ya Dk. Paul Lugata mganga mfawidhi  hospitali  ya Wilaya ya Mpanda

Nao baadhi ya wananchi wameeleza faida za kutumia maji mwilini ,wamewaomba wataalamu wa afya wazidi kutoa elimu sahihi ya matumizi sahihi ya unywaji wa maji ili jamii itambue faida za kutumia maji pamoja na hasara za kutotumia maji.

Sauti za wananchi