Rasilimali zilizopo Katavi fursa ukuaji uchumi kwa wananchi
24 September 2024, 8:47 pm
“Wapo wananchi ambao hawaelewi juu ya kuchangamkia fursa zinazopatikana mkoani Katavi”
Na Roda Elias-Katavi
Wananchi mkoani Katavi wameeleza namna wanavyonufaika na rasilimali zilizopo huku wakiiomba serikali kutatua baadhi ya changamoto .
Rasilimali zilizotajwa ni kama vile viwanda vidogo, uwepo wa Ziwa Tanganyika na mito mbalimbali huku ikielezwa kuwa vimekuwa chachu kubwa katika kukuza Kipato kwa wananchi.
Wakizungumza na Mpanda Radio Fm wananchi mkoani humo wamesema kuwa ipo haja ya kuweza kutatuliwa changamoto wanazozipata licha ya kupata faida kutokana na uwepo wa rasilimali hizo .
Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Katavi Anna Shumbi amesema kuwa wapo wananchi ambao hawaelewi juu ya uwepo wa fursa na kuchangamkia fursa hizo zinazopatikana mkoani humo hivyo ipo haja ya kutoa elimu juu ya rasilimali zilizopo na kuzitumia.
Katika hatua nyingine Shumbi amewataka wananchi kufuata taratibu na sheria kwani kila sekta iliyo na rasilimali za kimaendeleo kuna taratibu zake .