Mpanda FM

Katavi:Afisa muuguzi aondoa utata kati ya ugonjwa wa degedege na kifafa

13 September 2024, 12:56 pm

Rajabu Mollel Manaya afisa muuguzi Daraja la pili idara ya upasuaji na magonjwa ya ndani ya kina mama hospitali ya rufaa mkoani Katavi .picha na Rechel Ezekia

“Mitazamo yao kuhusiana na degedege kwa Watoto katika jamii huku wakihusianisha na imani za kishirikina

Na Rachek ezekia -Katavi

Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kufahamu tofauti kati  ya ugonjwa wa kifafa na degedege  ikiwa ni pamoja na kutohusianisha magonjwa hayo na Imani za kishirikina .

Akizungumza ofsini kwake Rajabu Mollel Manayaa afisa muuguzi Daraja la pili idara ya upasuaji na magonjwa ya ndani ya kinamama hospitali ya rufaa mkoani Katavi amesema kuwa  degedege inawapata Watoto wadogo na husababishwa na  kukosa hewa au kupata mgandamizo wakati wa kuzaliwa.

Sauti ya Rajabu Mollel muuguzi Daraja la pili idara ya upasuaji na magonjwa ya ndani ya kina mama hospitali ya rufaa mkoani Katavi

Katika hatua nyingine amebainisha kuwa Watoto kuweweseka husababishwa na mama kutomnyonyesha mtoto kwa wakati, mtoto kuwa na homa kali ,ameeleza kuwa endapo mgonjwa wa degedege akiwahishwa hospitali mapema anapata matibu yanayotibu tatizo hilo.

Sauti ya Rajabu Mollel muuguzi Daraja la pili idara ya upasuaji na magonjwa ya ndani ya kina mama hospitali ya rufaa mkoani Katavi

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wametoa mitazamo yao kuhusiana na degedege kwa Watoto katika jamii huku wakihusianisha na imani za kishirikina wameomba  wataalamu wa afya kutoa elimu kwa jamii ili wapate uelewa zaidi .

Sauti ya wananchi