Kata ya Mpanda Hotel yahamasishwa usafi
2 September 2024, 9:22 pm
picha na mtandao
“kuna baadhi ya watendaji wa serikali wamekuwa hawatoi ushirikiano katika suala la usafi jambo ambalo halipendezi.“
Na Edda Alias-Katavi
Wananchi wa Mtaa wa Mpanda hoteli manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha wanafanya usafi kwenye mazingira yanayowazunguka .
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa mtaa huo Christina Mshani wakati wa kilele cha kampeni ya usafi iliyoandaliwa na kikundi cha TRANS CARGO.
Sauti ya mwenyekiti wa mtaa huo Christina Mshani akizungumza
Ibrahim Msanda amabaye ni mwenyekiti wa kikundi cha TRANS CARGO amesema usafi umefanyika maeneo mbalimbali lengo likiwa ni kuhakikisha manispaa inakuwa safi.
Sauti ya Ibrahim Msanda amabaye ni mwenyekiti wa kikundi cha TRANS CARGO
Kwa upande wake mstahiki meya wa manispaa ya Mpanda Haidary Sumry ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kuna baadhi ya watendaji wa serikali wamekuwa hawatoi ushirikiano katika suala la usafi jambo ambalo halipendezi.
Sauti ya mstahiki meya wa manispaa ya mpanda Haidary Sumry
Kilele cha kampeni hiyo ya usafi kimefanyika Kata ya Mpanda hotel ambapo kata ya Kashaulili imeongoza kwa usafi huku kata ya Nsemulwa ikifanya vibaya katika usafi na kupewa kinyago.