Katavi: CCM kata ya Nsemulwa hawajaridhishwa na mkandarasi wa daraja
2 September 2024, 8:25 pm
“Hawajaridhishwa na mkandarasi wa ujenzi wa daraja la Tulieni kwani hajafuata maagizo ya chama ya kufanya marekebisho.“
Liliani Vicent -Katavi
Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Nsemulwa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamesema hawajaridhishwa na mkandarasi wa ujenzi wa daraja la tulieni kwani hajafuata maagizo ya chama ya kufanya marekebisho.
Wameyasema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hiyo ambapo mkandarasi ametakiwa kurudi kujenga kwa kiwango kinachotakiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo Alex Ngereza amesema mkandarasi alipewa maelekezo ya kufanya marekebisho lakini hajafanya hivyo ambapo hatua zitachukuliwa kwa manufaa ya wananchi.
Ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Kata ya nsemulwa ilianza tarehe 23 mwezi Agost ambapo wametembelea shule ya msingi tulieni na kilimani ,kituo cha afya ,daraja la tulieni na umaliziaji wa wodi za kinamama.