Mpanda Radio FM kujenga choo bora kwa kaya moja yenye uhitaji
23 July 2024, 4:38 pm
Mke na Mume wa kaya hiyo ambao wanauhitaji wa choo ambapo wanasaidiwa na majirani kwa sasa .picha John Mwasomola
“Kaya hiyo ambayo ni wazee na wanashindwa namna ya kumudu kupata choo bora kutokana na kutokuwa na watu wa kuwasaidia kwani watoto wao wote wamefariki“
Na Anna Milanzi -Katavi
Katika kuhakikisha hamasa ya ujenzi wa vyoo bora unaendelea mkoani Katavi Mpanda Radio FM imeanzisha Kampeni ya usafi wa mazingira inayokwenda kwa jina kumekucha Mpanda hotel kampeni ambayo imeenda sambamba na kuisaidia Kaya moja ambayo haina choo kabisa.
Kaya hiyo ambayo ni wakazi wa mtaa wa Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imejikuta ikiishi bila choo na kueleza kuwa majirani wanawasaidia kujihifadhi huku kukiwa na changamoto wanazozipitia kutokana na wao kutokuwa na choo
Akizungumza mara baada ya kuitembelea kaya hiyo Meneja wa Kituo cha Mpanda Radio Fm Restuta Nyondo amesema wameona ni vyema kuisaidia familia hiyo kuwajengea choo kutokana na Kaya hiyo kuwa ni wazee na hawana hata watoto wa kuwasaidia.
Sauti ya Meneja wa Kituo cha Mpanda Radio Fm Restuta Nyondo
Mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda Hotel Christina Mshani amesema ameipendekeza kaya hiyo ipate msaada wa kujengewa choo bora kutokana na kaya hiyo kutokuwa na msaada .
Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda Hotel Christina Mshani
Kutokana na taarifa hiyo waliyopatiwa ya kujengewa choo wameishukuru mpanda Radio FM kwa uamuzi huo
Sauti ya mmoja wa wanaoishi katika kaya hiyo