Mpanda FM

Zaidi ya hekta 2077 ya misitu hupotea kila mwaka mkoani Katavi

14 June 2024, 3:57 pm

Pichani ni shughuli mbalimbali ambazo zinahatarisha na kusababisha upotevu wa misitu ikiwamo shughuli za uchomaji mkaa, ukataji kuni kwa ajili ya matumizi ya kupikia pamoja na uchomaji wa matofali. Picha na mtandao

“Wananchi wanapaswa kuachana na matumizi ya nishati ya kupikia ambayo si safi na kujikita katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuweza kuokoa mazingira na afya ya mtumiaji wa nishati hiyo”

Na Betord Chove -Katavi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema kuwa zaidi hekta 2077 za misitu  mkoa wa Katavi hupotea kwa matumizi ya nishati isiyo safi.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya nishati safi yaliyofanyika mkoani hapa Katavi iliyoambatana na ugawaji wa mitungi ya gesi kwa baadhi ya wananchi kwa ajili ya matumizi ya kupikia, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema kuwa kiasi hicho hupotea kwa ajili ya matumizi ya nishati ya kupikia kama vile kuni, mkaa na uchomaji wa tofali.

Sauti ya RC Mrindoko akizungumza katika kongamano hilo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi.

Baadhi ya wananchi mkoani Katavi waliojitokeza katika maadhimisho hayo wameshukuru kuwepo kwa maadhimisho hayo kwa kuwajengea uwezo wa matumizi ya nishati safi ambapo inakwenda kusaidia kuachana na matumizi ya nishati chafu ambayo imekuwa ni sehemu pia ya uharibifu wa mazingira.

Sauti ya wananchi waliojitokeza katika kongamano hilo wakipongeza hatua hiyo na kuwaasa wengine kutumia nishati safi ya kupikia

Maadhimisho ya matumizi ya nishati safi yamefanyika kwa siku tatu kwa lengo la kuhamasisha na kutoa elimu juu ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.



.