Mpanda FM

Zaidi ya Milioni 100 Kukamilisha Ujenzi wa Shule Nsemurwa

25 October 2021, 5:49 pm

MPANDA

Halmashauri ya manispaa ya  mpanda mkoani katavi imetenga shilingi milioni mia moja kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa shule ya sekondari nsemulwa kabla ya kufika mwaka 2022.

Kauli hiyo imetolewa na meya wa manispaa ya  mpanda Aidary Sumry alipokuwa kwenye ziara ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya  manispaa na kueleza mikakati waliyonayo ili kufanikisha kupokea wanafunzi ifikapo mwaka 2022.

Sauti ya Meya Manispaa Mpanda.

Kwa upande wake afisa elimu sekondari manispaa ya  mpanda Enelia Lutungulu ameeleza kuwa shule ya sekondari nsemulwa ikikamilika itaondoa changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu.

Sauti ya Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Mpanda

Kata ya Nsemulwa haina shule ya sekondari licha ya sera ya elimu nchini inataka kuwa na shule ya sekondari kila kata.