Elimu ya Kinga rafiki yawafikia vijana halmashauri ya Nsimbo
3 June 2024, 5:37 pm
baadhi ya vijana halmashauri ya Nsimbo wakipata elimu ya kinga rafiki kutoka kwa wawezeshaji shirika lisilo la kiserikali SHIDEFA.picha na John Benjamin
“dhumuni kubwa la zoezi hilo ni kutoa elimu kwa vijana jinsi yakujikinga na maambukizi ya vizuri vya ukimwi. “
Na John Benjamin -Katavi
Zaidi ya wananchi 1300 katika kijiji cha Itenka na kitogoji cha Magula halmashauri ya Nsimbo wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wamefikiwa na kupatiwa elimu na huduma kinga rafiki kwa vijana kutoka shirika la SHIDEFA Mpanda.
Akizungumza katika zoezi hilo msimamizi wa huduma za kinga ngazi ya jamii kutoka shirika lisilo la kiserikali Shidefa Mpanda Cleophas Julias amesema kuwa dhumuni kubwa la zoezi hilo ni kutoa elimu kwa vijana jinsi ya kinga na maambukizi ya Ukimwi na kutoa vifaa vya kujikinga kama Kondomu pamoja na kuendesha zoezi la upimaji wa maambukizi hayo.
Sauti ya msimamizi wa huduma za kinga ngazi ya jamii kutoka shirika lisilo la kiserikali Shidefa Mpanda Cleophas Julias
Alex Magesa mratibu wa Ukimwi halmashuri ya Nsimbo Amepongeza shirika hilo la shidefa Mpanda kwa kufanya zoezi hilo ambapo ameleeza kuwa katika halmashauri ya Nsimbo hali ya maambukizi ipo asilimia 5.8 hivyo amewaomba wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya na kujikinga na ungonjwa huo wa ukimwi
Sauti ya Alex Magesa mratibu wa Ukimwi halmashuri ya Nsimbo Amepongeza shirika hilo la shidefa Mpanda kwa kufanya zoezi hilo
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliojitokeza katika maeneo hayo ya kijiji cha Itenka na kitogoji cha Magula katika halmashauri ya Nsimbo wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wameshukuru shirika hilo kwa kuwafikia na kutoa elimu na kwa jamii na kuwaomba kuendelea kuwatembelea mara kwa mara
Wananchi waliojitokeza katika maeneo hayo ya kijiji cha Itenka na kitogoji cha Magula katika halmashauri ya Nsimbo wilaya ya Mpanda
Shirika la Shidefa Mpanda ni shirika lisilo la kiserikali ambapo limekuwa likitoa huduma na elimu ngazi ya jamii katika masuala ya namna ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi na unyanyasaji wa kijinsia.