TAKUKURU Katavi yapokea malalamiko ya rushwa 41 kwa miezi mitatu
24 April 2024, 7:24 pm
Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa {TAKUKURU} mkoa wa Katavi Faustine Maijo akizingumza na waandishi wa habari picha na Ben Gadau
“Kuhusu malalamiko ya Rushwa Takukuru katika kipindi hicho cha miezi mitatu tumepokea malalamiko 41 yanayohusiana na vitendo vya rushwa katika ya malalamiko hayo 38 yalikuwa ni ya rushwa na matatu hatakuwa ya rushwa”
Na Ben Gadau – Katavi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imefatilia utekelezaji wa miradi mitano inayotekelezwa katika Mkoa wa Katavi yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 5.82.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Faustine Maijo amesema serikali imepeleka fedha katika maeneo hayo ndio maana Takukuru wanafatilia kwa karibu utekeleza wa miradi yote inayotekelezwa kwenye mkoa wa Katavi.
Sauti ya Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa katavi Faustine Maijo
Maijo amebainisha kuwa katika miradi hiyo waliyofatilia inaendele vizuri huku wakibaini ucheleweshaji wa malipo ya wakandarasi na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi .
Kuhusu malalamiko ya Rushwa amesema Takukuru katika kipindi hicho cha miezi mitatu wamepokea malalamiko 41 yanayohusiana na vitendo vya rushwa katika ya malalamiko hayo 38 yalikuwa ni ya rushwa na matatu hatakuwa ya rushwa .
Sauti ya Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa katavi Faustine Maijo
Katika hatua nyingine Mkuu Maijo amewaonya wale wenye tabia ya kuwatapeli wananchi kwa kujifanya wao ni maafisa kutoka Takukuru kuacha mara moja tabia hiyo.