Katibu Mkuu CCM atua Mpanda, asikiliza kero za wananchi
14 April 2024, 1:18 am
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Balozi Dkt.Emmanueli Nchimbi akizungumza na Wananchi na Viongozi Mbalimbali Katavi .Picha na Samwel Mbugi
“Serikali itaendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika kusimamia miradi yote ili iweze kuleta manufaa yaliyokusudiwa“
Na Samweli Mbugi-Katavi
Kero Mbalimbali za Wananchi zimesikilizwa katika Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Balozi Dkt.Emmanueli Nchimbi ambapo pia ametoa Salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Nchimbi amesema kuwa Rais Samia atafanya Ziara ya kikazi hivi karibuni ambapo amesema mkoa wa Katavi umekuwa Ngome imara ya Chama cha Mapinduzi kwa Miaka Mingi sasa.
Sauti ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Balozi Dkt.Emmanueli Nchimbi
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Katavi Iddy Kimanta amesema kuwa ziara hiyo imetumika kujifunza mengi ambayo yamesemwa na Viongozi walioambatana na ujio wa Katibu Mkuu CCM Taifa.
Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Katavi Iddy Kimanta
Nae Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ametoa salamu kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Serikali itaendelea kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kusimamia Miradi yote ili iweze kuleta Manufaa yaliyokusudiwa.
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko
Katika hatua nyingine Katibu wa Itikadi,Uenezi,na Mafunzo Amosi Makala amesikiliza Kero za Wananchi ambazo amesema kuwa kero 27 zote zina uwezo wa kutatulika bila kuondoka nazo ambapo zitabaki zinatatulika na viongozi wa idara husika.
Sauti ya Katibu wa itikadi,uenezi,na Mafunzo Amosi Makala akizungumza juu ya kero alizosikiliza
Katibu wa itikadi,uenezi,na Mafunzo Amosi Makala akizungumza na Wananchi Picha na Samwel Mbugi