Dkt. Nchimbi apokelewa Katavi kwa kishindo
13 April 2024, 11:18 pm
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt.Emmanuel Nchimbi akiwasili Katika uwanja wa ndege Mkoani Katavi kwa ajili ya ziara ya siku mbili Mkoani hapa .Picha na Samwel Mbugi
“ Amewataka Viongozi kuhakikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wanaweka Wagombea ambao wanajiuza kwa Wananchi na sio kuweka Wagombea watakaotakiwa kusafishwa“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt.Emmanuel Nchimbi na Wajumbe wake,Wamewasili Mkoani Katavi kwa Ziara ya Siku mbili.
Dkt. Nchimbi ameongozana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa,itikadi,uenezi na Mafunzo Amos Makalla na Katibu wa NEC, Organization Issa Ussi Haji Gavu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt.Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati wa Mapokezi yake.Picha na Samwel Mbugi
Akizungumza katika maeneo ya Viwanja vya CCM Mkoa, Issa Ussi Gavu amewataka Viongozi kuhakikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wanaweka Wagombea ambao wanajiuza kwa Wananchi na sio kuweka Wagombea watakaotakiwa kusafishwa
Sauti ya Katibu wa NEC, Organization Issa Ussi Gavu akizungumza na kuwataka Viongozi wa CCM mkoa wa Katavi wanawaweka Wagombea wanaostahili
Kwa upande wake Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, itikadi, Uenezi na Mafunzo Amos Makalla amesema kuwa utaratibu utakaotumika kusikiliza kero za Wananchi ni zile ambazo hazipo Mahakamani.
Sauti ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amos Makalla akizungumza
Dkt. Nchimbi ametoa salamu za Chama katika Ofisi za CCM mkoa wa Katavi ambapo amewashukuru Viongozi wa Serikali na Chama kwa kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Sauti ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt.Emmanuel Nchimbi akizungumza na kuwashukuru Viongozi wa Serikali na Chama
Dkt. Nchimbi ameteuliwa January 15 Mwaka huu kupitia kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Kilichoketi Visiwani Zanzibar kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu Hassan.