Walimu wakuu watoroka chama Katavi
26 March 2024, 12:42 pm
“Ikiwa ni mara ya kwanza kwa mkutano mkuu wa walimu wakuu wa shule za msingi mkoa wa Katavi uliofanyika katika ukumbi wa manispaa huku ukiambatana na mafunzo ya uongozi na taaluma,huku ikiambatana na kauli mbiu isemayo ‘‘Tekeleza Mikakati Boresha Elimu Katavi’’ Picha na Gladness Richard
Na Gladness Richard-katavi
Umoja wa walimu Wakuu wa shule za Msingi mkoa wa Katavi [TAPCHA] Wamesemaa moja ya changamoto zinazowakabiri kwenye umoja ni kuwepo kwa utoro kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho hicho.
Hayo yamebainishwa kwenye Taarifa ya umoja huo iliyosomwa na katibu wa chama cha walimu Dismas Bunga mbele ya mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa chama hicho na kuainisha changamoto zinazowakumba kuwa baadhi ya wakuu wa shule wamekuwa wagumu kuchangia chama hicho na pengine kutoshiriki shughuli zinzoratibiwa na chama hicho mfano Vikao vya halmashauri.
Pia katibu amesema wapo baadhi ya viongozi wa halmashauri ambao hawatambui mchango wa umoja wa chama hicho pamoja na kazi nzuri wanazozifanya za kuhakikisha mkoa wa katavi unapiga hatua kwenye sekta ya elimu hivyo wameomba kurekebishwa kwa lugha rafiki ya kujenga ili kuendelea kuwatia moyo kwa kazi wananzozifanya.
Sauti ya katibu wa chama cha walimu [TAPCHA] Dismas Bunga wakati akisoma risala na kubainisha changamoto hizo.
Katibu wa chama cha walimu [TAPCHA] Dismas Bunga wakati akisoma risala na kubainisha changamoto hizo. Picha na Gladness Richard
Kwa upande wake Afisa Elimu mkoa wa Katavi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo Upendo Rweyemamu amesema kuwa walimu wote wanatakiwa kuwa na umoja ambao utawasaidia kutatua changamoto zao na kuwapa mbinu za kufaulisha huku akisema ukiwa Mwalimu mkuu ni lazima kuingia ndani ya chama hicho na iwapo hujaridhia kujiunga unatakiwa kuandika barua kwa Mkurugenzi ili uachie nafasi uliyopewa.
Sauti ya Afisa Elimu mkoa wa Katavi Upendo Rweyemamu akijibu risala hiyo.
Afisa Elimu mkoa wa Katavi Upendo Rweyemamu wakati akijibu risala hiyo.Picha na Gladness Richard
Ikiwa ni mara ya kwanza kwa mkutano mkuu wa walimu wakuu wa shule za msingi mkoa wa Katavi uliofanyika katika ukumbi wa manispaa huku ukiambatana na mafunzo ya uongozi na taaluma,huku ikiambatana na kauli mbiu isemayo ‘‘Tekeleza Mikakati Boresha Elimu Katavi’’