MUWASA Yawafutia Madeni Wateja 602
19 November 2021, 12:41 pm
Jumla ya wateja 602 wa huduma ya maji wafutiwa madeni yao na mamlaka ya maji safi na mazingira Manispaa ya Mpanda Muwasa baada ya bodi kujilidhisha kuwepo kwa changamoto ya madeni hayo
Akizungumza na Mpanda Redio FM afisa biashara wa mamlaka ya maji safi na mazingira Naamani Mgoye amesema kuwa bodi imelidhia zaidi ya shilingi milioni 250 ambayo ni sawa na wateja 602 kufutiwa madeni kwa sababu ya changamoto ya awali kuwa baadhi ya maeneo yalikuwa na wateja ambao hawakufungiwa dira ya maji hali ambayo imepelekea mteja kupata bili ambayo sio sahihi na matumizi yake
Injinia Herman Nguki mhadisi wa mtandao wa maji na matengenezo mamlaka ya maji Mpanda Muwasa ameshukuru kuongezeka kwa mradi wa Korongo namba 2 ambapo umeweza kuongeza zaidi milimeta 2000 kwa siku na kupunguza adha za maji katika manispaa ya Mpanda kwani wameweza kuhudumia maeneo mengi tofauti na awali.
Aidha Injinia Herman amewaomba wananchi kuwa wepesi kutoa taarifa pindi wanapoona hitirafu yoyote ambayo inapelekea umwangikaji wa maji.