Joy FM

Baraza la madiwani lapitisha bajeti ya bilioni 35.7 Kasulu Mji

19 February 2025, 10:45

Madiwani katika halmashauri ya mji wa Kasulu wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani, Picha Hagai Ruyagila

Kaimu Mkuu wa Wilaya Kasulu Kanali Kanali Michael Ngayalina ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya Buhigwe amesema bajeti iliyopishwa ikawe chachu ya kuchochea maendeleo kupitia miradi mbalimbali

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma limepitisha bajeti ya shilingi bilioni 35.7 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo

Bajeti hiyo imepitishwa katika kikao maalum cha baraza la madiwani ili kutekeleza miradi ya maendeleo itakayosaidia wananchi katika halmashauri hiyo.

Akizungumza baada ya kusomwa kwa bajeti hiyo, Kaimu mwenyekiti wa halamshauri ya Mji Kasulu ambaye pia ni diwani wa kata ya Kumnyika Mh. Seleman Kwirusha amewashukuru madiwani waliopitisha bajeti hiyo sambamba na wakuu wa idara ambao wamekuwa chachu ya kufanikisha bajeti hiyo kupita bila changamoto yoyote.

Sauti ya Kaimu mwenyekiti wa halamshauri ya Mji Kasulu Mh. Seleman Kwirusha

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Michael Ngayalina ambaye ni mkuu wa wilaya Buhigwe amesema bajeti hiyo itasaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyopo ndani ya halmashauri hivyo ni vizuri kushirikiana ili kufanikisha miradi iliyopo inatekelezwa bila changamoto yoyote.

Sauti ya Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Michael Ngayalina ambaye ni mkuu wa wilaya Buhigwe

Nao baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao hicho cha bajeti akiwemo Shekhe wa msikiti wa Mwilamvya Maurid Ramadhani na Katibu wa chama cha demekrasia na maendeleo CHADEMA wilaya ya Kasulu Emmanuel Simon wamesema utekelezaji wa bajeti hiyo ndiyo chachu ya maendeleo ya Halmashauri ya mji wa Kasulu.

Sauti ya baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao hicho cha bajeti akiwemo Shekhe wa msikiti wa Mwilamvya Maurid Ramadhani