Kanisa la anglikana laahidi kuunga mkono serikali utoaji huduma
17 October 2024, 11:25
Askofu kanisa la Anglikana dayosisi ya western Tanganyika mkoa wa kigoma amesema kanisa lipo tayari kushiriki na kuunga juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu ya maendeleo.
Na Hagai Ruyagila- Kasulu
Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Mkoani Kigoma Limesema litaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania kwa namna inavyoboresha miundombinu ya barabara, Zahanati, vituo vya afya pamoja na hospital.
Hayo yameelezwa na askofu wa kanisa la anglikana dayosisi ya western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta wakati akizungumza na radio joy fm ambapo amesema serikali imeendelea kufanya mambo makubwa katika wilaya ya Kasulu na mkoa wa kigoma hasa katika suala la uboresha wa miundombinu ya barabara na huduma ya afya.
Sauti ya Askofu Kanisa la Anglikana dayosisi ya western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta
Aidha askofu Bwatta amesema kanisa la anglikana linaendelea kushirikiana kwa ukaribu na serikali hata kwenye huduma za kijamii kuhakikisha jamii inapata elimu iliyo bora na huduma ya afya katika hospitali zao ziizopo mkoani Kigoma.
Sauti ya Askofu Kanisa la Anglikana dayosisi ya western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta
Kwa upande wake Mchungaji Canon Simon Kituye mkurugenzi wa kanisa la Anglikana parish ya Nguruka wilayani Uvinza kanda ya mto maragarasi amesema hali ilivyokuwa mwanzo na sasa kutofauti mkubwa kwasababu serikali imejitahidi kuboresha miundombinu ya barabara kwa kuweka lami na kuboresha vituo vya afya.
Sauti ya Mkurugenzi wa kanisa la Anglikan Nguruka Canon Kituye
Nao wananchi wa wilaya ya Kasulu akiwemo Juius Lameck na George Mamboeo wameishukrani serikali ya awamu ya sita kwa kutimiza wajibu wake kuhakikisha jamii inapata huduma bora za uhakika.
Sauti za wananchi