Madiwani Kasulu mji wachagua makamu mwenyekiti
2 October 2024, 09:10
Madiwani katika halmshauri ya mji wa Kasulu Mkoani kigoma wamesema kuwa wataendelea kumuunga mkono makamu mwenyekiti aliyechaguliwa kwa mara ya nne ili kuahkikisha wanatekeleza na kusimamia shughuli za maendeleo ndani ya wilaya hiyo.
Na Emmanuel Kamangu – Kasulu
Baraza la Madiwani halamashauri ya mji kasulu mkoani kigoma wamemchagua Diwani seleman kwirusha kwa mara ya nne kuwa makamu mwenyekiti wa halamshauri hiyo.
Makamu mwenyekiti ambaye amechaguliwa kwa awamu ya nne Bw, kwirusha amewashukuru kwa dhati waheshimiwa madiwani kwa kumuamini huku akiwaomba ushirikiano madiwani wote ili kusukuma gurudumu la maendeleo kikamilifu.
Diwani wa kata ya nyasha Bw, Patrick Madaraka ni mmoja wa madiwani ambao wamempongeza Bw, Kwirusha kwa kushinda kiti hicho huku akiwasirihi madiwani wenzake wa ccm kushikamana na kuacha misuguano inayoweza kuchelewesha shuguli za maendeleo.
Aidha miongoni mwa viongozi ambao wamechaguliwa kwenye kamati tatu za kudumu za halmashauri ni pamoja na kamati ya uchumi , elimu na afya Diwani Emmanuel Gamuye, sambamba na kamati ya mpango mji ,ujenzi na mazingira diwani Ezron Budurege.