Namna ongezeko la watu linavyoathri uchumi wa kaya
24 September 2024, 12:27
Serikali imesema halmashauri nchini hazina budi kutumia matokeo ya sensa ya mwaka 2022 kwa ajili ya kupanga maendeleo ya watu, familia na taifa kwa ujumla.
Na Michael Mpunije – Kasulu
Inaelezwa kuwepo kwa idadi kubwa ya watu kwenye kaya hupelekea athari za Kushuka kiuchumi na kusababisha mkuu wa kaya hiyo kushindwa kutoa huduma muhimu kwenye familia.
Hayo yameelezwa Afisa takwimu mwandamizi kutoka ofisi ya taifa ya Takwimu makao.makuu dodoma Bw. Omary Mdoka wakati akizungumza katika mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika halmashauri ya mji wa kasulu
Bw.Omary ameeleza namna ongezeko la watu kwenye kaya linavyoathri kiuchumi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishina jenerali mstaafu wa jeshi la.zimamoto na uokoaji Thobias andengenye amesema wanaume wanatakiwa kushirikiana na wake zao katika kuongeza kipato cha familia.
Aidha Andengenye amezitaka halmshauri zote za Mkoa wa Kigoma kuhakikisha wanaweka mipango ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuzingatia Takwimu za sensa ya watu na makazi.