Nuru FM

Usiri ndani ya familia chanzo cha ukatili Iringa

22 March 2023, 9:09 am

Picha ikionesha kiashiria cha usiri. Picha kwa msada wa mtandao

Katika kukabiliana na matukio ya ukatili katika jamii, usiri umetajwa kusababisha matukio hayo kukithiri.

Na fabiola Bosco

Usiri ndani ya familia umetajwa kuwa sababu ya ongezeko la vitendo vya ukatili wa kingono na vipigo kwa watoto mkoani Iringa licha ya elimu kutolewa katika jamii.

Kwa mujibu wa afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Iringa Bi Suzan Nyagawa  watoto wamekuwa wakifanyiwa ukatili ndani ya familia huku wazazi na watu wanaowazunguka wakishindwa kutoa taarifa za matukio hayo .

CUE 001 SUZAN NYAGAWA

Sauti ya Suzan Ngagawa akizungumzia kuhusu usiri unavyochangia ukatili kwa watoto

Ameongeza kuwa ni vyema watoto wakatoa taarifa kwa viongozi wa serikali za mitaa na watu wa malezi ili kudhibiti vitendo hivyo .

“kwa kweli ni vyema wananachi wakawa wazalendo katika kutoa taarifa za ukatili zinapotokea katika maeneo yao” alisema Nyagawa

“kwa kweli ni vyema wananachi wakawa wazalendo katika kutoa taarifa za ukatili zinapotokea katika maeneo yao” alisema Nyagawa

Mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake wa kike alifanyiwa ukatili wa kingono anasema aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi ili kudhibiti vitendo hivyo .

sauti ya Mzazi wa Mtoto aliyefanyiwa ukatili wa kingono

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa Dkt. Arfred Mwakalebela kati ya watoto wawili hadi watatu wanaofikishwa hospitalini hapo kwa wiki wanakuwa wamefanyiwa ukatili wa kingono.

MWISHO