Nuru FM

Tanroads Iringa yaicharaza Njombe 5-0

28 February 2023, 4:58 pm

Viongozi wa Tanroads kutoka mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya wakati wa kukabidhi kombe.Picha na Ansigary Kimendo.

Katika kujenga mahusiano mazuri ya kiutendaji,TANROADS mkoa wa Iringa pamoja na mikoa ya Njombe na Mbeya wamefanya bonanza la michezo.

Na Ansigary Kimendo

TANROADS mkoa wa Iringa wamefanya bonanza la michezo lililoshirikisha watumishi wa TANROADS kutoka mikoa ya Njombe Mbeya na mwenyeji akiwa ni Iringa lengo likiwa ni kufahamiana na kujenga mahusiano mazuri baina yao.

Bonanza hilo lililofanyika siku ya Jumamosi tar 25.02.2023  kwenye  Viwanja vya Samora mkoani Iringa likijumuisha mchezo wa mpira wa pete kwa wanawake, na  mpira wamiguu kwa wanaume, ambapo Katika mchezo wa Mpira wa Miguu TANROADS mkoa wa Iringa waliibuka na ushindi wa magori 5-0 dhidi ya TANROAD Njombe.Huku mpira wa pete TANROADS mkoa wa Mbea wakishinda mabao 20-3 dhidi ya Iringa.

Akizungumza mara baada ya Mchezo huo kumalizika mchezaji kutoka timu ya TANROADS mkoa wa Njombe HADSON MTAGILA amesema kuwa mchezo huo ulikuwa mzuri na licha ya kufungwa na wao waliweza kuhamasika kuanzisha mabonanza hayo.

Tumefungwa lakini tunashukuru tumeweza kufahamiana na imetupa hamasha

Akizungumza mara baada ya Mchezo huo kumalizika mchezaji kutoka timu ya TANROADS mkoa wa Njombe Hadson Mtagila amesema kuwa mchezo huo umekuwa mzuri na licha ya kufungwa na wao wameweza kuhamasika kuanzisha mabonanza hayo.Tumefungwa kwenye mchezo wa miguu lakinitunashukuru tumeweza kufahamiana na imetupa hamasha nasisi kuanzisha mabinanza

Feby Raban kutoka timu ya TANROADS mkoa wa Mbeya ameeleza namna alivyofurahia bonanza hilo kwa kutoa nafasi  michezo mbalimbali ambayo imekuwa  haipewi kipaumbele ikilinganishwa na mpira wamiguu hasa mpira wapete ambapo timu hiyo iliweza kupata ushindi wa  mabao 20-3 dhidi ya Iringa.

Feby Raban kutoka timu ya TANROADS mkoa wa Mbeya akieleza namna alivyofurahia bonanza.

Kwa upande wake  ALEX MGONGOLWA ambae ni  mratibu wa michezo kutoka TANROADS mkoa wa iringa  alisema kuwa mambonanza hayo yatakuwa ni endelevu ambapo Tanroad mkoa wa Iringa watakwenda kushindana na mikoa mingine.

Mratibu wa michezo kutoka TANROADS mkoa wa Iringa Alex Mgongolwa akieleza mikakati ya bonanza.