Mpanda FM

Wananchi wanufaika na wiki ya sheria

3 February 2025, 6:58 pm

Picha ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa mkoa wa Katavi. Picha na Anna Mhina

“Mahakama ni chombo muhimu kwenye utoaji haki”

Na Lilian Vicent

Baadhi ya wananchi mkoani Katavi wamesema kuwa  kupitia wiki ya sheria wameweza kujifunza  sheria na kutambua haki zao ambazo walikuwa hawafahamu hapo awali.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda redio Fm katika viwanja vya mahakama ya hakimu mkazi Katavi na mahakama ya wilaya ya Mpanda ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria.

Sauti ya wananchi

Akimwakilisha mkuu wa mkoa wa katavi  Jamila Yusuph ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mpanda amesema kuwa mahakama ni chombo muhimu kwenye utoaji haki hivyo wana mchango mkubwa katika kufikia dira ya taifa ya maendeleo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mpanda

Kwa upande wake Gwaya Sumaye hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama mkoa Katavi amesema wamejipanga kuhakikisha  wanarejesha imani kwa wananchi kwa kuweka mifumo rafiki ya usikilizaji wa kesi.

Sauti ya Gwaya Sumaye

Maadhimisho ya wiki ya sheria yalianza January 25 na kilele chake kimefanyika  February 3 mwaka huu na kauli  mbiu isemayo Tanzania ya 2050 ,nafasi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya taifa ya maendeleo.