Wapishi wa migahawa watakiwa kuzingatia usafi
17 January 2025, 10:05 am
“Uchafu wa mazingira katika migahawa unaweza kusababisha magonjwa ya matumbo pamoja na kipindupindu “
Na Leah Kamala – Katavi
Wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Wamewataka wamiliki na wapishi wa migahawa kuzingatia usafi ili kujiepusha na ugonjwa wa Kipindupindu.
Wakizungumza na Mpanda Redio FM wamesema kuwa uchafu wa mazingira katika migahawa unaweza kusababisha ugonjwa wa kipindupindu kuenea kwa haraka na kuiomba serikali kusimamia sheria ili usafi uzingatiwe.
Daktari Gabriel Elias Lukubigwa Mratibu wa tiba Manispaa ya Mpanda amesema kuwa wamejipanga kuwatumia maafisa afya kupita maeneo yenye migahawa kuangalia kama wanazingatia kanuni za afya na lishe.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mpanda mkoani hapa Jamila Yusuph Kimaro amesema uuzaji wa vyakula maeneo ya shule haurusiwi ambapo wafanyabiashara wanapaswa kutafuta maeneo tofauti na shule kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa kipundupindu.