Wananchi washauriwa kuacha kula udongo
16 January 2025, 11:48 am
“Wameainisha sababu zinazowapelekea kutumia udongo“
Na Roda Elias-Katavi
Wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuacha ulaji wa udongo [maarufu kama Pemba ] ili kulinda afya na kuepukana na magonjwa.
Wakizungumza na Mpanda Redio FM wananchi hao wameainisha sababu zinazowapelekea kutumia udongo, huku wakionekana kutokujua madhara ambayo yanatokea kutokana na ulaji wa udongo .
Kwa upande wake afisa lishe manispaa ya Mpanda Neema Kambi, amewashauri wanawake ambao wameathirika na ulaji wa udongo,Wanapaswa kula chakula jamii ya wanyama pamoja na matunda ili kuwa na madini chuma katika miili Yao.
Kwa mujibu wa tafiti kutoka chuo kikuu kishiriki cha elimu mkwawa [MUCE] tafiti hiyo inaeleza udongo unaoliwa una madhara kiafya kwa kuwa unamejaa fangasi na bacteria hivyo kuhatarisha afya, moja ya watafiti profesa Joseph Ndunguru amesema lengo la tafiti hizo ni kusaidia jamii kutatua changamoto zinazowakabili