Mpanda FM

Wajasiriamali wahamasishwa kuchukua mikopo ya 10%

9 January 2025, 9:41 am

wajasiriamali mbalimbali katika soko dogo la machinjioni .picha na Roda Elias

kina mama, vijana pamoja na wazee wanapaswa kutambua faida za kujiunga na mikopo inayotolewa ya asilimia 10

Na Roda Elias -Katavi

Wajasiriamali  katika soko la masaa linalopatikana kata ya Mpanda Hotel wametakiwa kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa  ya asilimia 10.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika soko la masaa lililopo kata ya Mpanda Hotel ambapo ajenda kuu ilikuwa ni kusikiliza kero za wajasiliamali , Diwani wa kata ya Mpanda Hotel Hamisi Misigalo amesema kuwa kina mama, vijana pamoja na wazee wanapaswa kutambua faida za kujiunga na mikopo inayotolewa ya asilimia 10.

Akijibu swali la mmoja wa wajasiliamali diwani huyo amesema  kuwa amejitolea kuweka kiasi cha fedha katika mikopo, hivyo wajasiliamali wanapaswa Kuchukua mkopo na kurejesha kwa wakati ili waweze kupata tena mkopo .

Sauti ya diwani kata Mpanda Hotel

Diwani kata ya Mpanda Hotel.picha Roda Elias

Kwa upande wao baadhi ya kinamama wajasiliamali wamesema kuwa wapo tayari kuchukua mikopo na kuifanyia kazi ili kuzalisha faida.

Sauti ya wajasiriamali wakizungumza

Soko hilo la masaa ambalo wajasiliamali wake huuza na kunuua bidhaa kuanzia majira ya saa kumi na mbili asubuhi na kumalizika saa tano lilianza mnamo mwaka 2019.