Mpanda FM

DC Mpanda ahimiza utunzaji wa mazingira

16 December 2024, 10:41 am

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph aliye upande wa kulia akiwa katika picha ya pamoja na Oswald Laswai ambaye ni meneja wa TFS wilaya ya Mpanda pamoja Samwel Mbugi kushoto mwandishi wa habari Mpanda Radio FM

Wameandaa miti 7500 kwa kupanda katika tasisi mbalimbali za umma na wananchi binafsi ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani”

Na Samwel Mbugi -Katavi

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ambae amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko katika zoezi la ugawaji na upandaji miti amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na taasisi mbalimbali zilizojitokeza katika shule ya msingi Mkapa ambapo zoezi la upandaji miti limefanyika na kusema kuwa zoezi hilo litasaidia kujikinga na Madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph

Kwa upande wake Oswald Laswai meneja wa TFS wilaya ya Mpanda amesema katika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania wameandaa miche tofauti tofauti ili kuigawa kwa wananchi lengo likiwa ni kutunza mazingira na kuboresha afya za wananchi.

Sauti ya Oswald Laswai meneja wa TFS wilaya ya Mpanda

Nae afisa misitu Manspaa ya Mpanda Peter Lupeja amesema kuwa wameandaa miti 7500 kwa kupanda katika tasisi mbalimbali za umma na wananchi binafsi ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani.

Afisa misitu Manispaa ya Mpanda Peter Lupeja

Maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanafanyika kila December 9, na kwa mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo uongozi Madhubuti na ushirikishwaji wa wananchi ni msingi wa maendeleo yetu.