RC Katavi ahamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura
27 November 2024, 3:48 pm
“Mrindoko amewataka wananchi Kuendelea kujitokeza katika vituo mbalimbali walivojiandikisha ili kuweza kujitokeza ili kutimiza haki yao ya kupiga kura.”
Na Betord Chove -Katavi
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko Ameshiriki kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Ilembo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Akizungumza na waandishi wa habari Mrindoko amewataka wananchi Kuendelea kujitokeza katika vituo mbalimbali walivojiandikisha ili kuweza kujitokeza ili kutimiza haki yao ya kupiga kura.
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza
Kwa Upande wao baadhi wa wananchi waliojitokeza kupiga kura katika kituo cha Ilembo wamepongeza utaratibu ulivyowekwa na kuwataka wananchi ambao bado hawajajitokeza kwenda ili jkuweza kupiga kura.
Sauti za Wananchi waliojitokeza kupiga kura
Kwa upande wake Rebeka Msambusi mratibu wa uchaguzi ngazi ya mkoa amesema maandalizi ya uchaguzi yamekamilika katika vituo vyote mkoani hapa.
Sauti ya Rebeka Msambusi mratibu wa uchaguzi ngazi ya mkoa
Ikumbukwe Mikoa yote nchini inapiga kura November 27 katika uchaguzi wa serikali za mitaa