Wakulima Katavi wahimizwa kutambua afya ya udongo
27 November 2024, 3:06 pm
“Wakulima wanapaswa kufuata elimu inayotolewa na wataalam kupitia vyeti vyao ili kuweza kuvuna mazao mengi zaidi“
Na John Benjamin -Katavi
Wakulima katika kata ya Itenka halmashauri ya Nsimbo wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kulima kisasa kwa kufuata maelekezo ya watalaamu wa kilimo.
Hayo yamebainishwa na katibu Tawala wilaya ya Mpanda Jofrey Mwashitete katika hafla ya kukabidhi vyeti vya afya ya udongo kwa baadhi ya wakulima katika kijiji cha Imilamate ambapo ameleeza kuwa kupitia vyeti hivyo wakulima wanapaswa kufuata elimu inayotolewa na wataalamu kwa kupitia vyeti vyao ili kuweza kuvuna mazao mengi zaidi.
Sauti ya katibu Tawala wilaya ya Mpanda Jofrey Mwashitete
Akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi Rodrick Mtulo amesema kuwa halmashauri ya Nsimbo kuanzia mwezi juni hadi kufikia tarehe 22 mwezi 11 mwaka huu wakulima 508 wamepimiwa udongo katika mashamba yao huku kata ya Itenka jumla ya wakulima 205 tayari wamekwisha pimiwa mashamba yao.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa kata ya Itenka halmashauri ya Nsimbo wameshukuru serikali kupitia wizara ya kilimo kwa zoezi hilo kwani linakwenda kuwasaidia katika shughuli zao za kilimo.
Sauti ya wakulima wa kata ya Itenka halmashauri ya Nsimbo
Serikali kupitia wizara ya kilimo ilianzisha mfumo wa upimaji wa afya ya udongo na kugawa vitendea kazi kwa halmashauri zote nchini kwa ajili ya kuhakikisha wakulima wanatambua afya za udongo kwenye mashamba yao na wanajua namna ya kutatua ili waweze kupata mazao mengi.