Mpanda FM

RC Katavi ahimiza haki katika uchaguzi wa serikali za mitaa

25 November 2024, 3:03 pm

mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvu Mrindoko akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.picha na Samwel Mbugi

kila mwananchi aliyejiandikisha ana haki ya Kwenda kuchagua kiongozi anayemuona ataweza kumtumikia kwa miaka mitano.

Na Samwel Mbugi -Katavi

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewahimiza wananchi wa mkoa wa Katavi waliojiandikisha katika daftari la mkazi kujitokeza kupiga kura November 27,2024 katika vituo walivyojiandikisha.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake November 25,2024 ambapo amesema kila mwananchi aliyejiandikisha ana haki ya Kwenda kuchagua kiongozi anayemuona ataweza kumtumikia kwa miaka mitano.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi

Mrindoko amewataka wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa Kutenda haki kwa vyama vyote vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo iliyowekwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Sauti ya mkuu wa mkoa akisisitiza wasimamizi kutenda haki

Hata hivyo Mrindoko amewahakikishia wananchi wote wa mkoa wa Katavi usalama katika kipindi chote cha kampeni na siku ya uchaguzi, ambapo amesema mkoa uko salama na  wamejipanga vizuri katika kuhakikisha amani inatawala siku zote.