Wasimamizi Nsimbo watakiwa kuzingatia kanuni za uchaguzi
25 November 2024, 1:16 pm
“Wametakiwa kuhakikisha wanasimamia ipasavyo muda sahihi wa kufungua na kufunga vituo vya kupigia kura “
Na Betord Chove -Katavi
Wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya vituo halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia muda wa kufungua na kufunga vituo vya kupigia kura kama ambavyo sheria na taratibu zinavyotaka
Akizungumza mara baada ya kufunga mafunzo hayo msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Nsimbo Stephano Kaliwa amewataka washiriki kuzingatia kanuni na sheria walizoelekezwa ili kufanya uchaguzi wa amani na haki.
sauti ya Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Nsimbo Stephano Kaliwa
Wakizungumza baada ya kula kiapo baadhi ya washiriki wameeleza matarajio yao ni kufanya vizuri katika usimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa november 27.
Sauti ya washiriki
Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Mikoa yote ya Tanzania bara November 27 mwaka huu.