Mpanda FM

Katavi: Wanufaika wa mradi wa TASAF wapongezwa kwa kazi wanazozifanya

16 November 2024, 6:59 pm

Naibu Waziri ofisi ya Rais Utumishi na utawala bora Deus Sangu ambae ni Mbunge wa jimbo la Kwela mkoa wa Rukwa picha na Samwel Mbugi

“wanufaka wa mradi wa TASAF wanafanya kazi kwa bidii kwa kukarabati miundombinu ikiwemo ya barabara”

Na Samwel Mbugi -Katavi

Naibu Waziri ofisi ya Rais Utumishi na utawala bora Deus Sangu ambae ni Mbunge wa jimbo la Kwela mkoa wa Rukwa amewapongeza wanufaika wa mradi wa TASAF kwa kazi wanazofanya za kujitolea ikiwemo ujezi wa Barabara.

Ameyasema hayo November 16,2024 wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza katika kata ya Ilembo iliyopo Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi kuwa wanufaika wa mradi wa TASAF wamezitendea haki fedha zinazowafikia kwa kufanya maendeleo.

Sauti ya naibu Waziri ofisi ya Rais Utumishi na utawala bora Deus Sangu ambae ni Mbunge wa jimbo la Kwela mkoa wa Rukwa

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ambae amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ametoa shukurani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha ili kuzinufaisha kaya maskini.

Sauti ya mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ambae amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akizunumza mbele ya Naibu waziri huyo akiwamwakilisha mkuu wa mkoa wa Katavi .picha na Samwel Mbugi

Baadhi ya wanufaika wa mradi wa TASAF wameeleza namna walivyonufaika na mradi huo kwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba na kusomesha Watoto wao.

Sauti ya Naibu Waziri ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Deus Sangu

Hata hivyo Naibu Waziri ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Deus Sangu amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassani ameanzisha mpango wa kuwakopesha wanufaika wa TASAF mikopo yenye riba nafuu katika vikundi vyao.