Mpanda FM

Katavi:Wataalamu wa kilimo watakiwa kutoa elimu ya kilimo kwa wakulima

17 October 2024, 10:32 am

Picha na mtandao

“Wamejipanga kuhakikisha wakulima wanalima kilimo chenye tija kwa kutumia mbinu bora zitakazosaidia kuzalisha kwa tija.”

Na Lilian Vicent -Katavi

Baadhi ya wakazi mkoani Katavi wamewataka wataalamu wa kilimo kuendelea kutoa elimu kwa wakulima ili kuhakikisha uzalishaji wa mazao unazidi kuongezeka.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Redio FM ikiwa ni maadhimisho ya chakula duniani ambayo hufanyika kila October 16 ya kila mwaka.

Sauti za wakulima wakizungumza

Faridu Mtiru afisa kilimo mkoani Katavi amebainisha kuwa wamejipanga kuhakikisha wakulima wanalima kilimo chenye tija kwa kutumia mbinu bora zitakazosaidia kuzalisha mazao kwa tija.

Sauti ya afisa kilimo mkoa wa Katavi

Kwa upande wake  mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema licha ya uzalishaji mwingi mkoani humo bado kuna hali ya udumavu hivyo wamejipanga kuendelea kutoa elimu.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi