Mpanda FM

Wananchi Katavi waomba watoto waishio mazingira hatarishi wasaidiwe

6 October 2024, 12:30 pm

picha na mtandao

serikali itoe  Elimu kwa wazazi kuhusiana  na malezi bora kwa mtoto na kuwapa mikopo wazazi ili kuwasaidia kukidhi mahitaji madogo madogo kama vile kumpeleka mtoto shule,malazi na chakula ili Watoto waepukane na makundi hayo hatarishi.

Na Edda Enock -Katavi

Baadhi ya Wananchi manispaa ya Mpanda  mkoani Katavi wameiomba serikali kuwasaidia Watoto ambao wanajiunga na makundi hatarishi na hatimae kujihusisha na uporaji na unyang’anyanyi.

Wakizungumza na Mpanda radio FM  wananchi hao wamesema kuwa serikali itoe  Elimu kwa wazazi kuhusiana  na malezi bora kwa mtoto na kuwapa mikopo wazazi ili kuwasaidia kukidhi mahitaji madogo madogo kama vile kumpeleka mtoto shule,malazi na chakula ili Watoto waepukane na makundi hayo hatarishi.

Sauti ya wananchi wakizungumza

Hayo yanajiri kufuatia kauli ya Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko aliyoitoa September 28/2024 katika viwanja vya polisi Buzogwe ambapo alipiga marufuku Watoto kutokujihusisha na makundi hatarishi

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi akizungmza