Mpanda FM

Katavi:Kiongozi wa mbio za mwenge”miradi iendane na thamani ya pesa”

13 September 2024, 11:59 am

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa katika picha akiwa na viongozi wengine wilaya ya mpanda akiwemo mkuu wa wilaya ya mpanda Jamila Yusuph.picha na Betord Chove

Wajibu wa watekelezaji wa mradi huo pamoja na serikali kuhakikisha jengo hilo linakuwa na thamani kama iliyoainishwa ya shilingi milioni 110.

Na Betord Chove -Katavi

Kiongozi wa Mbio za mwenge Kitaifa mwaka 2024 Geodfrey Mnzava Amewataka Viongozi wa serikali wilayani Mpanda kujiridhisha thamani ya pesa ilyotumika katika Ujenzi wa Nyumba mbili [two in one] katika shule ya Sekondari Kawalyoha.

picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wilaya ya Mpanda pamoja na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa .picha na Betold Chove

Akizungumza mara baada ya kukagua ili kuweza kuzindua nyumba hizo Mnzava amesema  Lengo la serikali ni kuleta mradi huo ili walimu waweze kupata makazi ili kulitumikia taifa kwa weredi hivyo ni wajibu wa watekelezaji wa mradi huo pamoja na serikali kuhakikisha jengo hilo linakuwa na thamani kama iliyoainishwa ya shilingi milioni 110.

Sauti ya Kiongozi wa Mbio za mwenge Kitaifa mwaka 2024 Geodfrey Mnzava

 Awali Akizungumza kwa niaba ya wananchi,Mbunge wa Jimbo la Mpanda Sebastiani Kapufi ameshukuru serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuendelea  kuboresha  mazingira ya walimu ili waweze kufanya kazi kwa weledi.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Mpanda Sebastiani Kapufi

Katika hatua nyingine Mnzava akiwa katika manispaa ya Mpanda amefungua klabu ya kupinga madawa ya kulevya na rushwa katika shule ya sekondari Magamba, klabu  ya kupinga ukatili katika shule ya sekondari Mwangaza,na kutembelea kituo cha afya cha Kazima na kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kugawa vyandarua, na mitungi ya gesi.

 Mwenge wa uhuru umekimbizwa  manispaa ya Mpanda September  12 na September 13 utakabidhiwa wilaya ya Tanganyika na  Kauli mbiu ya m bio za Mwenge kitaifa kwa mwaka 2024 ni “tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu.