Wananchi Katavi watoa mapendekezo dira ya maendeleo ya taifa 2025-2050
13 August 2024, 7:02 pm
Baadhi ya wananchi manispaa ya mpanda mkoa wa katavi .picha na Samwel Mbugi
“Serikali ya Tanzania iliandaa na kuridhia kutumika kwa Dira ya taifa ya maendeleo ya 2025 ampapo utekelezaji wake umewezesha nchi kupata mafanikio mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.”
Na Samwel Mbugi-Katavi
Baadhi ya wananchi manispaa ya mpanda mkoa wa Katavi wametoa mapendekezo yao juu ya dira mpya itakayoanza kutumika mwaka 2025 hadi 2050 kwa njia ya dodoso na mazungumzo katika ukumbi wa manispaa mkoa wa Katavi ambapo mwenyekiti wa zoezi hilo alikuwa mkuu wa wilaya ya mpanda Jamilla Yusuph.
Badhi ya maoni ambayo yametolewa na Richard Eliasi Mponega katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA amesema kuwa anatamani kuona Tanzania yenye siasa safi ambayo iliasisiwa na Baba wa taifa Nyerere na kuitengenezea misingi kipindi cha uhai wake.
Sauti ya Richard Eliasi Mponega katibu cha chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA
Kwa upande wake afisa mipango na Uchumi manispaa ya Mpanda Leonard Kilamuhama amesema serikali ya Tanzania iliandaa na kuridhia kutumika kwa Dira ya taifa ya maendeleo ya 2025 ambapo utekelezaji wake umewezesha nchi kupata mafanikio mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Sauti ya afisa mipango na Uchumi manispaa ya Mpanda Leonard
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamilla Yusuph ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho amesema kuwa dira inayotekelezwa mpaka sasa ni ya mwaka 2000 hadi 2025 ambapo kumeshuhudiwa mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya.
Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamilla Yusuph
Hata hivyo mkuu wa wilaya amesema kila kitu kinachotekelezwa na serikali kinalenga kufikia vipaumbele na malengo makuu ya dira ya taifa ya mwaka 2025