TAKUKURU Katavi yaitaka jamii kutojihusisha na vitendo vya Rushwa wakati wa uchaguzi
30 July 2024, 1:19 pm
kamanda wa taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa katavi Stuart Kiondo .Picha na Betord Chove
“taasisi hiyo imejipanga kutoa elimu Kwa wananchi na wanaopanga safu za uongozi,wagombea Ili waweze kutambua madhara ya rushwa“
Na Betord Chove -Katavi
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Katavi imeitaka jamii kutojihusisha na vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa baadae mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa Habari naibu kamanda wa taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa katavi Stuart Kiondo Wakati akitoa taarifa kuanzia mwezi april mpaka June 2024 amesema taasisi hiyo imejipanga kutoa elimu Kwa wananchi na wanaopanga safu za uongozi,wagombea Ili waweze kutambua madhara ya rushwa.Aidha Kiondo mesema Katika kuongeza elimu Kwa umma taasisi hiyo Katika kipind Cha April June wametembelea na kuimarisha klabu 25 za wapinga rushwa Ili kukuza kizazi chenye uadilifu na kupunguza rushwa nchini hasa Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Sauti ya kamanda wa taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa katavi Stuart Kiondo
Katika Hatua nyingine Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU ) mkoani Katavi kuanzia April Hadi June imefuatilia utekelezaji wa miradi nane yenye thamani ya billion 8.91 Katika sekta ya elimu,uchumi,biashara na miundombinu Ambapo imebaini ucheleweshaji wa miradi,malipo ya wakandarasi na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi.
Sauti ya kamanda wa taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa katavi Stuart Kiondo