Katavi :Bilion moja kutolewa kwa wasanii halmashauri ya Nsimbo
30 July 2024, 11:55 am
Afisa mtendaji mkuu mfuko wa utamaduni na sanaa Tanzania Nyakaho Mturi Mahemba .picha na Samwel Mbugi
“amewataka wananchi kuacha kukopa mikopo ya kausha damu kwani imekuwa ikirudisha maendeleo nyuma kwa wananchi.“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Afisa mtendaji mkuu mfuko wa utamaduni na sanaa Tanzania Nyakaho Mturi Mahemba ameahidi kutoa Tshs bilioni moja ili kuwakopesha wasanii kwa riba nafuu katika jimbo la Nsimbo.
Ameyasema hayo alipotembelea kata ya Itenka, Ibindi na Machimboni na kuongeza kuwa mikopo hiyo inaanzia kiasi cha shillingi laki mbili hadi milioni mia moja kwa msanii mmoja mmoja hadi kikundi.
Sauti ya Afisa mtendaji mkuu mfuko wa utamaduni na sanaa Tanzania Nyakaho Mturi Mahemba
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Nsimbo Anna Richard Lupembe ametoa shukrani kwa mkurugezi wa mfuko wa utamaduni kwa kukubali kufika jimbo la Nsimbo na kuahidi kutoa kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuwainua wasanii wa jimbo lake.
Sauti ya mbunge wa jimbo la Nsimbo Anna Richard Lupembe
Kwa upande wake afisa wa Benk ya CRDB branch ya Mpanda Ernest Benedict Ernest amesema vigezo vya kupata mkopo huo ni kufungua acoount ambayo utatakiwa kuwa na kitambulisho cha nida au leseni ya gari.
Sauti ya afisa wa Benki ya CRDB branch ya Mpanda Ernest Benedict Ernest
Hata hivyo afisa mtendaji mkuu mfuko wa utamaduni na sanaa Tanzania Nyakaho Mturi Mahemba amewataka wananchi kuacha kukopa mikopo ya kausha damu kwani imekuwa ikirudisha maendeleo nyuma kwa wananchi.