Mpanda FM

Kutoeleweka dhana ya 50 kwa 50 chanzo cha malezi ya mzazi mmoja mkoani Katavi

16 July 2024, 9:43 am

Picha na Mtandao

malezi ya mzazi mmoja  na Wamekuwa wakitoa elimu katika jamiii ili Watoto wapate malezi ya wazazi   pande zote.

Na Rachel Ezekia-Katavi

Kufuatia takwimu za zinazoonesha ongeza la Watoto wanaolelewa na mzazi mmoja, Wazazi na walezi  Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa  kuhakikisha wanawalea Watoto katika misingi bora ya malezi.

 Akizungumza na Mpanda Redio Fm Afisa ustawi wa jamii Thabiti Mlagano  amebainisha kuwa dhana ya uelewa duni ya 50 kwa 50 inapelekea ongezeko la malezi ya mzazi mmoja katika jamii huku akiwataka wazazi na walezi kuiilewa dhana hiyo ili isiathiri malezi ya Watoto.

Sauti ya Afisa ustawi wa jamii Thabiti Mlagano

Aidha ameongeza kuwa takwimu zinaonesha kuwa manispaa ya Mpanda kumekuwa na kesi  za malezi ya mzazi mmoja  na Wamekuwa wakitoa elimu katika jamiii ili Watoto wapate malezi ya wazazi   pande zote.

Sauti ya afisa ustawi manispaa

Kwa upande wao baadhi  ya wananchi  wamesema kuwa hali ya kipato na  wanaume kudharaulika inapelekea wanawake kuwalea  Watoto kwa nguvu zao wenyewe huku wakiamini kuwa malezi bila baba yanawezekana.