RC Katavi aagiza kufanyika tathmini kutofikia malengo zao la pamba
4 June 2024, 4:02 pm
Mrindiko ameagiza kuhakikisha malengo ambayo yanapangwa yanafikiwa kwa wakulima kufuata mbinu za kilimo na wataalam kuhakikisha tathmini inafanyika ili kulinganisha na misimu mingine kwanini imekuwa vigumu kufikia lengo la kuzalisha tani milioni 50 Picha na Festo Kinyogoto
Na Festo kinyogoto-katavi
Wakulima wa zao la pamba, tumbaku na mazao mchanganyiko mkoani Katavi wamehakikishiwa soko la uhakika la mazao hayo pamoja na malipo kwa wakati ili kujikimu na kukuza uchumi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindiko katika hafla ya uzinduzi wa msimu wa masoko ya pamba, tumbaku na mazao mchanganyiko iliyofanyika katika kijiji cha Makongoro kata ya Magamba halmashari ya Manisapaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Mrindiko amesema katika ushirika ambao unanunua mazao mkoani hapa Katavi kampuni ya GBS haijawahi kuwa na changamoto ya ulipaji hivyo ni chachu kwa wakulima kuendelea kuzalisha kwa wingi ili kujikimu binafsi na kukuza uchumi wa mkoa.
Awali akitoa tathmini ya kilimo kwa mkoa wa Katavi kaimu katibu tawala wa mkoa wa Katavi Nehemia James amesema mkoa umefanikiwa kuzalisha kilo milioni 12 Kwa mwaka huu huku sababu ya uazalishaji huo ikiatajwa kuwa ni uwepo wa kiwanda kimoja kilichopo halmashari ya wilaya ya Tanganyika pamoja na maji kutuama, magonjwa shambulizi na wakulima kutofuata mbinu za ugani.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa zao hilo wamesema uwepo wa soko hilo unatoa hamasa ya uzalishaji kwao kwa kuwa hawatapata ugumu wa kuuza mazao pale unapofikia muda wa mavuno licha ya kuwa bei ipo chini hivyo wamewaomba wanunuzi kuongeza bei ili waweze kunufaika zaidi.
Mrindiko ameagiza kuhakikisha malengo ambayo yanapangwa yanafikiwa kwa wakulima kufuata mbinu za kilimo na wataalam kuhakikisha tathmini inafanyika ili kulinganisha na misimu mingine na kwanini imekuwa vigumu kufikia lengo la kuzalisha tani milioni 50.