Simba Yasemekana Kuonekana Maeneo ya Mpanda Hotel na Msasani
16 May 2024, 4:46 pm
“Tumepokea barua kutoka kambi ya Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ ikimuarifu kuwajulisha wananchi wa mtaa wake kuwepo kwa mnyama Simba ili wawe makini pindi wanapokuwa katika shughuli zao hususani zile za usiku Amesema mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda hotel. Picha na mtandao
Na Samwel Mbugi-katavi
Wananchi wa kata Mpanda Hotel Manispaa Ya Mpanda mkoa wa Katavi wameiomba serikali kufanya jitihada za haraka kuhakikisha Mnyama Simba ambae ameonekana mtaa wa Msasani na mtaa wa Mpanda Hotel, kuwindwa haraka na kurudishwa Hifadhini.
Wameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wa Mpanda Hotel kuwa wamepokea taarifa hizo kutoka kwa viongozi wao wa serikali za mtaa, ambapo wameiomba mamlaka husika kulishughulikia swala hilo kabla madhara hayajatokea kwa Wananchi.
Sauti ya Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wa Mpanda Hotel
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda Hotel Christina Mshani amesema kuwa amepokea barua kutoka kambi ya Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ ikimuarifu kuwajulisha wananchi wa mtaa wake kuwepo kwa mnyama Simba ili wawe makini pindi wanapokuwa katika shughuri zao hususani zile za usiku.
Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda Hotel Christina Mshani akimesema kuwa amepokea barua kutoka kambi ya Jeshi la Polisi JWTZ ikimuarifu kuwajulisha wananchi wa mtaa wake kuwepo kwa mnyama Simba.
Nae Mwenyekiti wa mtaa wa Msasani Juvenaly Deusi amesema kuwa amewajulisha Wananchi wake kuwa mtaa wake kuna taarifa za kuwepo kwa Mnyama Simba kwa kupiga mbiu amboyo imeweza kumfikia kila Mwananchi wa mtaa huo.
Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Msasani Juvenaly Deusi
Hata hivyo Afisa wa KANAPA Beny Mbuya amesema kuwa bado hawajapata tarifa hizo za uwepo wa Mnyama Simba katika maeneo hayo yaliyotajwa na viongozi wa Serikali za mitaa husika.
Sauti ya Afisa wa KANAPA Beny Mbuya akimesema kuwa bado hawajapata tarifa hizo za uwepo wa Mnyama Simba katika maeneo hayo.